• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujerumani wailaza Ukraine 2-0 kwenye EURO

    (GMT+08:00) 2016-06-13 09:35:38

    Mabingwa wa dunia Ujerumani wameanza vyema harakati zao za kulisaka kombe la ulaya UERO kwa kuitandika Ukraine.

    Ujerumani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ambayo yalifungwa na Shkodran Mustafi dakika ya 19 na Bastian Schweinsteiger dakika ya 90.

    Kwa muda wote wa dakika 90 Ukraine walionekana kuwa wanyonge na Ujerumani kuzidi kumiliki mpira kwa asilimia 63, huku Ukraine wakilimilki kwa asilimia 37.

    Kwa sasa Ujerumani wanaongoza Kundi C kwa kuwa na pointi 3 na magoli mawili wakifuatiwa na Poland wenye pointi tatu na goli moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako