• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mambo wanayotakiwa kujua watu wanaopenda kula pilipilihoho

    (GMT+08:00) 2016-06-13 14:28:36

    Katika majira ya joto, watu wengi hutaka kula chakula chenye pilipilihoho ili ziweze kuongeza ladha zaidi, lakini baada ya kula viungo hivyo kwa vingi, watu wengi huwa na dalili ya kuumwa na koo hata kuhara, njia gani nzuri ya kuweza kula pilipilihoho bila kuharibu miili yetu? Wataalamu wa lishe ya chakula wanashaurii kwamba:

    Kwanza, bora ule pilipilihoho mbichi badala ya kutumia mafuta yanayotengenezwa na kiungo hicho, kwani ukitumia mafuta ya kiasi sawa na pilipilihoho yenyewe, basi kwa kweli, unakuwa unakula kiasi kingi zaidi cha pilipilihoho;

    Pili, ukila pilipilihoho, bora utie siki kidogo kwenye mlo wako, kwani siki inaweza kupunguza uwasho wake na kupunguza athari ya kiungo hicho mwilini.

    Tatu, unaweza kuchagua matunda kama vile matufaa au pea ambayo yanaweza kusaidia kulainisha koo lako na pia unaweza kunywa mtindi kidogo ili kulinda utumbo wako.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako