• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege ya kwanza duniani ya abiria isiyo na rubani iliyosanifiwa na China kufanyiwa majaribio nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2016-06-15 14:15:05

    Bw. Tom Wilczek, ofisa wa safari ya ndege na viwanda vya ulinzi wa ofisi ya maendeleo ya uchumi ya jimbo la Nevada, Marekani, amesema ofisi yake na taasisi ya mitambo inayojiendesha yenyewe ya Nevada NIAS zimesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya ndege zisizo na rubani ya Ehang iliyoko huko Guangzhou, China. Pande mbili zitashirikiana katika majaribio, usanifu na mafunzo kuhusu ndege ya abiria isiyo na rubani.

    Taasisi ya NIAS itaisaidia kampuni ya Ehang kufanya majaribio ya ndege ya abiria isiyo na rubani iitwayo "Ehang 184", kuomba idhini kwenye idara ya safari ya ndege ya Marekani. Majaribio ya ndege hiyo yatafanyika katika uwanja wa ndege zisizo na rubani ulioko katika jangwa la jimbo hili mwaka huu.

    Siku hizi miradi mbalimbali ya teknolojia ya hali ya juu ikiwemo teknolojia ya reli ya kasi ya HyperloopOne inatekelezwa jimboni Nevada. Bw. Wilczek alisema serikali ya Nevada imetambua moyo wa uvumbuzi wa kampuni hiyo ya China, na inaona kuwa ndege ya abiria isiyo na rubani ina mustakabali mzuri, pia inapenda kushirikiana na kampuni ya China kuendeleza ndege ya aina hiyo.

    Mwezi Januari mwaka huu kampuni ya Ehang ilionesha ndege ya "Ehang 184" kwenye maonesho ya bidhaa za elektroniki huko Las Vegas, na kuwavutia wataalamu wengi kutoka Nevada.

    Jina la "Ehang 184" linamaanisha kuwa ndege hiyo inaweza kubeba abiria mmoja, ina rafadha nane na mikono minne. Umbo lake linafanana na helikopta na inaweza kujiendesha yenyewe bila ya rubani. Kampuni ya Ehang inatarajia kuwa ndege hiyo itatumiwa na watu katika maisha yao ya kila siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako