• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukubwa wa ngisi unaweza kufikia mita ngapi?

    (GMT+08:00) 2016-06-15 14:20:04

    Ngisi mkubwa aina ya Architeuthis ni samaki mkubwa zaidi asiye na uti wa mgongo. Mwanabiolojia wa Chuo Kikuu cha St. Andrews Dr. Chris Paxton alisema tangu ngisi wa aina hiyo wagunduliwe, watu wengi wameweza kukisia ngisi mkubwa zaidi ana ukubwa gani.

    Mwanabiolojia huyu ametafiti rekodi za sampuli za ngisi wakubwa, na kukadiria urefu mkubwa zaidi unaweza kufikiwa na ngisi wa aina hiyo kwa hatua mbalimbali, zikiwemo kupima urefu wa mdomo na kichwa. Amesema kichwa kirefu zaidi kina urefu wa mita 2.79, anakadiria kuwa urefu wa ngisi huyu ni mita 14.28. Lakini tokeo hili halimaanishi ngisi mkubwa zaidi duniani ana urefu huo. Kwanza, urefu wa vichwa vya ngisi tofauti huenda unachukua asilimia tofauti ya urefu kamili; pili, ngisi aliyegunduliwa huenda si mkubwa zaidi duniani, kwa sababu wale wakubwa wanaishi katika bahari zenye kina kirefu sana ambako binadamu hawawezi kufika, huenda wale wakubwa zaidi bado hawajagunduliwa.

    Dr. Paxton alisema, akifikiri tofauti ya urefu wa vichwa vya ngisi mbalimbali, anakadiria kuwa urefu wa ngisi wenye kichwa cha mita 2.79 ni kati ya mita 5.83 na mita 27.52. Hii inamaanisha kuwa urefu wa baadhi ya ngisi pengine unaweza kufikia zaidi ya mita 20, hata zaidi ya mita 27.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako