• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajimu wamegundua sayari kubwa zaidi inayozunguka nyota mbili.

    (GMT+08:00) 2016-06-15 14:33:55

    Wanajimu wa Marekani wakitumia darubini ya anga ya juu ya Kepler wamegundua sayari kubwa zaidi inayozunguka nyota mbili. Mtu akisimama kwenye sayari hiyo, ataona mandhari ya ajabu yenye majua mawili.

    Sayari maarufu zaidi inayozunguka nyota mbili huenda ikawa ni sayari ya Tatooine inayosimuliwa kwenye filamu ya Starwars. Sayari hiyo ni makazi ya familia ya Skywalker. Kutua kwa majua mawili ni mandhari inayokumbukwa na watazamaji wengi katika filamu hiyo. Hivyo wanajimu pia wanaziita Tatooine sayari za aina hiyo. Mwaka 2011, wanajimu waligundua kwa mara ya kwanza sayari ya aina hiyo, ambayo imepewa jina la Kepler-16b.

    Sayari mpya iliyogunduliwa imepewa jina la Kepler-1647b, iko katika kundi la nyota la Cygnus ambalo liko umbali wa miaka 3700 ya kusafiri kwa mwanga kutoka dunia yetu. Sayari hiyo ina umri wa miaka bilioni 4.4, ambao ni karibu sawa na dunia yetu, na pia iko kwenye ukanda unaofaa maisha ya viumbe, lakini hali nyingine hazifanani kabisa na dunia yetu.

    Watafiti wa idara ya safari za anga ya juu ya Marekani NASA na Chuo kikuu cha San Diego wametoa ripoti wakisema sayari hiyo inaundwa na hewa, uzito na ukubwa wake unafanana na sayari ya Jupiter, hivyo viumbe haviwezi kuishi juu yake. Lakini kama kungekuwa na satilaiti za mwamba zinazoizunguka, huenda viumbe vingeweza kuishi huko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako