• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huwezi kujifunza lugha ya kigeni kwa urahisi? Ni tatizo la jeni yako!

    (GMT+08:00) 2016-06-16 15:11:18

    Kwa nini baadhi ya watu wanajifunza lugha ya kigeni kwa urahisi, lakini wengine wanaona ni vigumu kujifunza? Utafiti mpya uliotolewa kwenye gazeti la taasisi ya sayansi ya Marekani unaonesha kuwa uwezo wa kujifunza lugha huenda unahusiana na jeni.

    Wanafunzi 79 wa China wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Washington kwa mwaka wa kwanza wameshiriki kwenye utafiti huo. Wastani wa umri wa wanafunzi hao ni miaka 20, na wote hawajawahi kuishi ng'ambo.

    Wanafunzi 44 walipewa mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa wiki tatu, na wengine 35 hawakupewa. Baadaye watafiti wa chuo hiki walichunguza neva zinazohusiana na uwezo wa lugha za ubongo wa wanafunzi hao kwa teknolojia ya Diffusion Tensor Imaging. Neva zinazofanya kazi vizuri zinawafanya watu wawe na uwezo mkubwa zaidi wa kujifunza lugha nyingine. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa wanafunzi waliopewa mafunzo ya lugha kwa muda mrefu zaidi, neva zinafanya kazi vizuri zaidi. Lakini uwezo wa kujifunza wa baadhi ya wanafunzi bado ukawa mdogo kuliko wengine.

    Watafiti wametafiti DNA za wanafunzi hao, na kugundua kuwa jeni iitwayo COMT inahusiana na mabadiliko ya ubongo wao baada ya kupewa mafunzo. Jeni hiyo inasaidia kudumisha kiasi cha kemikali za Dopamine na Norepinephrine kwenye ubongo wa binadamu. Na utafiti mpya unaonesha kuwa mabadiliko mawili yakitokea kwenye jeni hiyo, uwezo wa kujifunza lugha unaongezeka. Kwa ujumla jeni hiyo inaathiri asilimia 46 ya uwezo wa kujifunza lugha ya kigeni.

    Watafiti wataendelea kutafiti sababu nyingi zinazoathiri uwezo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako