• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vinywaji vimoto huenda vikasababisha saratani ya umio

  (GMT+08:00) 2016-06-20 10:26:59

  Idara ya utafiti wa saratani ya kimataifa IARC ya Shirika la Afya Duniani imetangaza kuwa kunywa vinywaji vimoto zaidi ya nyuzi 65 sentigredi vinaweza kusababisha saratani ya umio, na imekanusha maoni ya zamani kwamba kawaha inaweza kusababisha saratani kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha.

  Dk. Christopher Wild wa idara hiyo Amesema kunywa vyinywaji vimoto vikiwemo maji, kahawa, chai kutaongeza hatari ya kupata saratani ya umio, sababu sio vinywaji vyenyewe, bali ni ujoto mkubwa. Katika nchi zilizoendelea, sababu kuu ya saratani hiyo ni kuvuta sigara na kunywa pombe, lakini saratani hiyo inatokea kwa wingi katika nchi za Asia, Amerika Kusini na Afrika Mashariki. Desturi ya pamoja ya nchi hizi ni kunywa vinywaji vimoto.

  Idara hiyo iliwahi kuweka kahawa kwenye orodha ya vitu vyenye uwezekano wa kusababisha saratani. Lakini utafiti mwingi umeonesha kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unaoweza kuthibitisha maoni hayo, bali kahawa inawasaidia binadamu kukinga magonjwa mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako