• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wa China na Marekani wavumbua teknolojia mpya ya kutatua uchafuzi wa takataka za plastiki

    (GMT+08:00) 2016-06-21 09:49:34

    Wanasayansi wa China na Marekani wametangaza kuvumbua teknolojia mpya ya kuozesha takataka za plastiki aina ya Polyethylene, kemikali zinazotolewa baada ya plastiki kuoza zinaweza kutumiwa kuzalisha dizeli.

    Kikundi kinachoongozwa na Dr. Huang Zheng cha taasisi ya kemikali ya kikaboni ya Shanghai na kikundi kinachoongozwa na Guan Zhibing cha tawi la Irvine la Chuo Kikuu cha California, Marekani vimeshirikiana kuvumbua teknolojia hii.

    Uchafuzi wa takataka za plastiki ni tatizo gumu linalokabiliwa na nchi mbalimbali. Zaidi ya tani milioni 100 za plastiki aina ya Polyethylene zinazalishwa kila mwaka duniani. Lakini ni vigumu sana kwa plastiki hiyo kuoza katika mazingira ya kiasili. Hivi sasa takataka nyingi za plastiki zinazikwa au kuteketezwa, lakini kuzikwa kunahitaji eneo kubwa la ardhi na kutasababisha uchafuzi wa maji chini ya ardhi, na kuteketezwa kutatoa hewa nyingi za Carbon Dioxide na uchafuzi mwingine.

    Wanasayansi wametumia kemikali aina ya alkane yenye kaboni chache kuharakisha plastiki kuoza. Kemikali hiyo inazalishwa kwa wingi katika mchakato wa kusafisha mafuta ghafi, lakini haiwezi kutumiwa kama mafuta au gesi ya asilia, hivyo haina thamani kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako