• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uefa yaipiga faini ya euro 100,000Croatia baada ya mashabiki kufanya fujo

    (GMT+08:00) 2016-06-21 10:30:34

    Uefa imeipiga faini Croatia euro 100,000 baada ya mashabiki wake kufanya fujo katika mchezo uliochezwa Ijumaa na kutoka sare ya 2-2 dhidi Jamhuri ya Czech kwenye michuano ya Euro 2016. Pia Shirikisho la Soka la Croatia limepigwa marufuku kuwauzia tiketi mashabiki na kutajwa kuwa ni wahuni. Lakini kwa vile tiketi za mechi ya leo dhidi ya Uhispania tayari zimeshauzwa, hivyo marufuku hii imeahirishwa hadi mwisho wa mashindano. Hata hivyo kama mashabiki wataleta tena fujo katika mechi ya leo ambayo ni ya mwisho kwenye kundi D, marufuku hivyo itatekelezwa mara moja. Faini hiyo ni ya pili kwa ukubwa kutolewa kwenye mashindano baada ya Russia kupigwa faini ya euro150,000 wiki iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako