• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lionel Messi avunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote ya staa wa zamani wa Argentina Gabriel Batistuta

    (GMT+08:00) 2016-06-23 09:10:25

    Jana nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi alivunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote ya staa wa zamani wa Argentina Gabriel Batistuta, baada ya kufunga goli la faulo dakika ya 32 katika mchezo dhidi ya Marekani na kufikisha jumla ya magoli 55 na kumzidi Batistuta kwa goli moja. Lionel Messi amekuwa mfungaji wa mara zote wa Taifa la Argentina, baada ya kuiongoza nchi yake kuifunga Marekani mabao 4-0 na kuingia hatua ya fainali ya michuano ya Copa America. Messi alifunga bao lake la 55, kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa NRG , na kuipiku rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mfungaji wa zamani Gabriel Batistuta mwenye mabao 54. Mchezaji huyo mara tano wa dunia, hadi sasa amefunga mabao 5, kwenye michuano hiyo ya Copa America, na ana nia ya kuisaidia Argentina kutwaa taji hilo, walilolikosa kwa miaka 23 hadi sasa. Argentina huenda ikakutana na Chile au Colombia kwenye fainali hiyo itakayopigwa jumapili hii kwenye uwanja wa East Rutherford, New Jersey.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako