• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kufanya mazoezi ya viungo katika wakati mwafaka kunasaidia kuinua uwezo wa kukumbuka

    (GMT+08:00) 2016-06-23 14:59:18

    Watafiti wa Uholanzi wametoa makala kwenye gazeti la Current Biology la Marekani wakisema kufanya mazoezi ya viungo saa 4 baada ya kujifunza, kunasaidia kuinua uwezo wa kukumbuka. Lakini kufanya mazoezi mara moja baada ya kujifunza hakusaidii.

    Watafiti wa Taasisi ya ubongo, ufahamu na vitendo ya Donders ya Uholanzi waliwataka watu 72 waliojitolea kujifunza kukamilisha picha za mahali 90 ndani ya dakika 40. Baadaye watu hao waligawanywa katika vikundi vitatu. Kikundi kimoja kilifanya mazoezi ya viungo mara moja, kingine kilifanya mazoezi baada ya saa 4, na kingine hakikufanya mazoezi. Njia ya kufanya mazoezi ilikuwa ni kupanda baiskeli.

    Baada ya siku mbili, watu hao walifanya mtihani kuhusu picha hizi, na ubongo wao ulipimwa kwa teknolojia ya MRI ili kujua sehemu gani za ubongo wao zinachangamka zaidi. Matokeo yanaonesha kuwa watu waliofanya mazoezi ya viungo saa 4 baada ya kujifunza wamekumbuka picha nyingi zaidi, na wale waliofanya mazoezi mara moja wamekumbuka picha chache zaidi kuliko wale ambao hawakufanya mazoezi. Upimaji wa ubongo unaonesha kuwa sehemu ya Hippocampus ya ubongo wa wale waliofanya mazoezi saa 4 baada ya kujifunza inachangamka zaidi. Sehemu hiyo inahusiana na uwezo wa kukumbuka na kujifunza.

    Watafiti wamesema kukumbuka ujuzi kunahitaji kemikali maalum ndani ya ubongo wetu zikiwemo Dopamine na Norepinephrine. Watu wanaofanya mazoezi ya viungo, utoaji wa kemikali hizi unaongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako