• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzalishaji wa nafaka huenda utapungua ndani ya muongo ujao

    (GMT+08:00) 2016-06-23 14:59:42

    Watafiti wametafiti ukuaji wa mahindi barani Afrika ukiathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Prof. Andy Challinor wa Chuo Kikuu cha Leeds cha Uingereza amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa si kama tu yamesababisha kuongezeka kwa joto barani Afrika, bali pia yamesababisha ukame kutokea mara kwa mara. Mambo hayo yataathiri uzalishaji wa mahindi barani humo.

    Watafiti wametafiti athari ya joto katika ukuaji wa mahindi, na kugundua kuwa hali ya hewa ikiwa ya joto zaidi, muda wa ukuaji wa mahindi utakuwa mfupi, lakini uzalishaji utapungua.

    Watafiti wamekadiria kuwa ifikapo mwaka 2018, muda wa ukuaji wa mahindi utakuwa mfupi katika baadhi ya maeneo barani Afrika, na ifikapo mwaka 2031, hali hii itatokea katika maeneo mengi barani Afrika. Nchi za Afrika zinatakiwa kufanya juhudi zote kukuza aina mpya ya mahindi yanayoweza kukabiliana na mabadiliko ya hewa ndani ya muongo ujao, ama sivyo uzalishaji wa mahindi utaathirika kwa kiasi kikubwa.

    Mabadiliko ya hali ya hewa pia yataathiri mazao mengine ya kitropiki, lakini kwa kawaida kukuza aina mpya ya mazao na kuwahimiza wakulima kuyalima kunahitaji muongo mmoja hadi mitatu. Watafiti wamependekeza nchi mbalimbali ziharakishe kukuza na kusambaza mazao mapya kwa kuboresha teknolojia za kilimo na utaratibu wa kuidhinisha mauzo ya mazao mapya sokoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako