• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Sunway TaihuLight" imekuwa kompyuta inayohesabu kwa kasi zaidi duniani

    (GMT+08:00) 2016-06-23 15:00:46

    Orodha mpya ya kompyuta 500 zinazohesabu kwa kasi zaidi imetangazwa hivi karibuni. "Sunway TaihuLight" inayotumia chip zilizotengenezwa na China kwa kujitegemea imechukua nafasi ya kwanza badala ya "Tianhe-2". Na idadi ya kompyuta za China zilizowekwa kwenye orodha hiyo kwa mara ya kwanza imechukua nafasi ya kwanza badala ya Marekani.

    "Sunway TaihuLight" inaweza kuhesabu mara trilioni elfu 93 kwa sekunde, si kama tu kasi yake ni karibu mara mbili ya ile ya "Tianhe-2", bali pia ufanisi wake umeongezeka mara tatu. Muhimu zaidi ni kwamba "Tianhe-2" inatumia chip zilizotengenezwa na kampuni ya Intel, lakini kompyuta hiyo inatumia chip zilizosanifiwa na kutengenezwa na China.

    "Sunway TaihuLight" ilisanifiwa na kituo cha utafiti wa teknolojia za kompyuta zinazofanya kazi nyingi kwa wakati mmoja cha China, imewekwa kwenye kituo cha supakompyuta mjini Wuxi. Kabla ya hapo "Tianhe-2" iliyosanifiwa na Chuo Kikuu cha sayansi na teknolojia ya ulinzi cha China ilichukua nafasi ya kwanza kwenye orodha hiyo kwa miaka 6 mfululizo.

    Kompyuta 10 zinazohesabu kwa kasi zaidi ni pamoja na "Sunway TaihuLight", "Tianhe-2", "Titan" na "Sequoia" za Marekani, "K" ya Japan, "Mira" na Trinity" za Marekani, "Piz Daint" ya Uswisi, "Hazel Hen" ya Ujerumani na "Shaheen II" ya Saudi Arabia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako