• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CPU yenye core elfu moja inayotumia nishati chache yasanifiwa

    (GMT+08:00) 2016-06-23 15:01:05

    CPU za kompyuta zetu zina core mbili, nne au nane ili kukidhi mahitaji ya kufanya kazi mbalimbali kwa wakati mmoja. Hata baadhi ya simu za mkononi zinatumia CPU zenye core kumi. Hivi karibuni watafiti wa tawi la Davis la Chuo Kikuu cha California wamesanifu CPU iitwayo Kilocore ambayo ni ya kwanza duniani yenye core elfu moja, na inaweza kufanya kazi nyingi zaidi kwa kutumia nishati chache.

    CPU hiyo ina transista milioni 621, inaweza kutekeleza maagizo trilioni 1.78 kwa sekunde, na imetengenezwa kwa teknolojia ya CMOS yenye ukubwa wa nanomita 32 ya kampuni ya IBM.

    Prof. Bevab Bass anayeongoza kikundi cha usanifu wa CPU hiyo amesema CPU hiyo inaweza kufanya kazi nyingi zaidi kwa kutumia nishati chache kuliko CPU nyingine, ufanisi wake ni mara 100 ya CPU ya laptop. CPU hiyo ikitekeleza maagizo bilioni 115 kwa sekunde, inahitaji umeme wa watt 0.7, hivyo betri moja aina ya AA inatosha mahitaji yake. Msanifu wa CPU hiyo Bw. Brent Bohnenstiehl alisema kila core inafanya kazi yenyewe, hivyo core zisizofanya kazi zinaweza kuzimwa kwa muda ili kubana matumizi ya nishati.

    Kabla ya CPU hiyo kusanifiwa, ingawa CPU zenye core nyingi zimetumiwa kwa wingi, lakini idadi ya core haijawahi kuzidi 300, tena kwa kawaida CPU zenye core nyingi sana zinatumiwa kwa utafiti tu, hazitumiwi kutengeneza bidhaa za eletroniki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako