• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufisadi waota mizizi katika bandari ya Dar es salaam

    (GMT+08:00) 2016-06-23 20:05:28

    Serikali ya Tanzania imebaini ufisadi mkubwa katika mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ya Tanzania (TPA) kutokana na kukamilika kwa kazi ya Tume iliyoundwa kuchunguza utendaji wa kazi wa mamlaka hiyo, na imeagiza hatua kali ichukuliwe dhidi ya watu wanaohujumu Bandari ya Dar es Salaam.

    Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Tanzania Bw Makame Mbarawa amesema baadhi yao wanatakiwa kwanza kufikishwa mbele ya taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi lakini akionya kuwa ni marufuku kwa wahusika kupewa barua za onyo.Aidha Bw Makame amesema ufisadi mwingine umebainika katika miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambapo mingi imewekwa ili kuwanufaisha watu na si serikali, mgongano mkubwa wa maslahi kwa Bodi ya Zabuni uliochangia kukwama kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo, ajira za kindugu, kulindana, mtandao wa wezi, rushwa na uwezo mdogo wa kiutendaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako