• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TFF yasema imeshawalipa wachezaji wa Taifa Stars

    (GMT+08:00) 2016-06-24 08:32:41

    Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF limekanusha madai ya kutokuwalipa wachezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars mara baada ya kuvunjwa kwa kambi ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Chad pamoja na mchezo dhidi ya Misri. Afisa habari wa TFF Alfredy Lucas amesema, kuhusu madai ya posho ya kambi ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ya kuwania kufuzu kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Chad ambayo Chad walijitoa katika mashindano walishaongea na wachezaji na wakaelewana kwani hela wanazotakiwa kulipwa wachezaji wa Stars zinatakiwa kulipwa na Chad.

    Na kuhusu mchezo wa Taifa Stars na Misri, Lucas amesema mara baada ya kumalizika kwa mchezo, Rais wa TFF Jamal Malinzi alimuomba kocha wa Stars Charles Boniface Mkwasa kuelekea kambini na wachezaji ambapo walikabidhiwa posho zao. Lucas ameonya kuwa taarifa zanazosambazwa na baadhi ya watu kwa madai ambayo sio ya kweli zinalenga kuharibu wachezaji ambao mwisho wa siku watashindwa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako