• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanariadha wa Kenya na Russia watakiwa wathibitishe kama wako safi ili washiriki Olimpiki ya Rio

    (GMT+08:00) 2016-06-24 08:33:09

    Wanariadha wa Kenya na Russia wanaotaka kushindana kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio wameambiwa wathibitishe kuwa wako safi hawatumii dawa za kuongeza nguvu na wamepewa siku 11 kufanya hivyo. Mataifa hayo mawili yamesimamishwa kwenye michuano ya kimataifa kwa kukiuka sheria za kutumia dawa zilizopigwa marufuku na shirika la WADA. Hata hivyo Kamati ya Olimpiki ya kimataifa itawaruhusu kushindana mwaka huu kwenye michezo ya Rio kama watafaulu baada ya kupimwa tena. Mamlaka za Kenya na Russia zimeomba kupatiwa ufafanuzi zaidi na IOC juu ya wanariadha wao watawezaje kufuzu na kushiriki michuano hiyo. Lakini kama washiriki watakao faulu baada ya kupimwa tena wataiwakilisha nchi yao au la hilo bado halijafahamika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako