• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Sekta ya kilimo yapokea msaada wa bilioni 173

    (GMT+08:00) 2016-06-24 17:24:35

    Katika jitihada zake za kuimarisha kilimo ili kubuni ajira na kuchangia maendeleo ya Uchumi nchini humo,Rwanda imepata msaada wa fedha wa shilingi bilioni 173 kutoka kwa muungano wa Ulaya .

    Fedha hizo zitatumika kuinua sekta ya kilimo katika miaka ijayo.

    Serikali ya Rwanda imetia sahihi fedha hizo zitakazobadilisha sekta ya kilimo.

    Waziri wa fedha na Uchumi Rwanda Claver Gatete amesema watabuni miradi kukuza chakula katika jamii za mashinani na kupanua kilimo kupitia kwa uzalishaji bora.

    Serikali ya Rwanda imesemaitasaidiana na wakulima kwa kuweka mipango ya unyunyizaji maji na kuanzisha kilimo cha misitu ili kuvuta mvua.

    Wwakulima wataanzishiwa vyama vya ushirika na mikopo ili kupata fedha za kujiendeleza pamoja na kukabiliana na changamoto za kilimo.

    Wakulima watapewa fedha za mtaji pia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako