• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Hazina ya biashara kupunguza ajira miongoni mwa vijana

    (GMT+08:00) 2016-06-24 17:24:35

    Hazina ya biashara nchini Rwanda imetakiwa kutafuta mbinu za kubuni ajira ili kupunguza idadi ya vijana ambao hawana ajira Rwanda.

    Waziri wa Biashara na viwanda Francois Kanimba amesema serikali itaweka mikakati ya kufikia malengo yake ya Uchumi kwa kuanzisha maendeleo ya kazi ndogo ndogo na wastani.

    Hazina hiyo itaanza kutoa fedha kwa vijana ambao hawana elimu ya kutosha kwa kuwapatia boda boda na kuwaaanzishia biashara ndogo ndogo za jua kali ili wajikimu kimaisha.

    Vijana watapewa mikopo kuanzisha biashara hizo kupitia kwa vikundi.

    Wilaya 30 itapata fedha hizo kwa kupendekeza miradi yao ya Biashara .

    Mkurugenzi wa hazina hiyo Inocent Bulundi amesema mipango kabambe itawekwa kufanikisha mradi huu mkubwa Rwanda.

    Bulindi amesema kupitia miradi hii wanatarajia vijana elfu 23,700 katika kila wilaya kupata ajira .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako