• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Bei ya unga sima kupanda Kenya,Rwanda na Uganda

    (GMT+08:00) 2016-06-24 17:24:35

    Wateja wa Unga wa mahindi watalazimika kutumia fedha zaidi kufuatia ongezeko la bei ya bidhaa hiyo.

    Nchini Rwanda bei ya unga wa mahindi imepanda kutokana na kupungua kwa mahindi na kuongezeka kwa mahitaji.

    Hali hiyo pia imeshuhudiwa Kenya baada ya wizara ya kilimo kuthibitisha kwamba kutakuwa na kasoro ya mahindi kutokana na msimu mbaya wa mvua mwaka huu.

    Kenya imetegemea mahindi ya Tanzania ambayo yanuzwa kwa bei ya juu.

    Ripoti ya wizara ya kilimo imebainisha kasoro hii ikieleza kwamba bei ya mahindi itapanda kwa shilingi 15 kwa kilo.

    Sasa gunia moja la mahindi kutoka Daresalaam ni shilingi 2700 Nairobi ,4500 Uganda na 4597 Burundi.

    Wazalishaji wa mahindi wamelalamikia upungufu wa mavuno uliopunguza bidhaa hiyo kwa wamiliki wa viwanda vya usagaji.

    Kenya imekumbwa na kasoro ya magunia milioni 20 ya mahindi.

    Kilo moja ya unga sima ni shilingi 110 kutoka 95 na inatarajiwa kupanda zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako