• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Museveni kufufua kampuni ya ndege ya Uganda

    (GMT+08:00) 2016-06-24 17:24:35

    Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda ametoa agizo la kufufuliwa kwa kampuni ya ndege ya Uganda.

    Museveni ameitaka wizara ya uchukuzi kuanda majadiliano na wawekezaji ili kutafuta mbinu ya kifufua kampuni hiyo.

    Katika kikao chake cha kwanza na baraza la mawaziri ,Museveni amesema ni aibu kwa Uganda kukosa shirika la ndege la kitaifa .

    Uganda imekuwa ikitegemea mashirika ya nje ya ndege kuingia na kutoka nchini humo jambo ambalo wanauchumi wanasema linaikosoesha nchi hiyo mapato.

    Kampuni ya Uganda Airlines imekosa kufanya huduma zake kwa mwongo mmoja sasa.

    Hii ni baada ya kukumbwa na deni kubwa la shiulingi bilioni 21 za Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako