• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Russia wakutana

    (GMT+08:00) 2016-06-24 20:29:24

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake Vladmir Putin wa Russia wamekutana mjini Tashket kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kuboresha nafasi ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai katika maendeleo ya kanda na usalama.

    Rais Xi amesema, ziara ya rais Putin ina umuhimu wa kipekee kwa kuwa huu ni mwaka wa 15 tangu China na Russia zisaini mkataba wa ujirani mwema wa kirafiki na ushirikiano, na pia ni mwaka wa 20 wa kumbukumbu ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa nchi hizo mbili.

    Kwa upande wake, rais Putin ametoa salamu zake za rambirambi kutokana na vifo na hasara zilizosababishwa na dhoruba kubwa iliyoukumba mkoa wa Jiangsu. Pia amesema atatumia ziara yake nchini China kubadilishana maoni kwa kina na rais Xi kuhusu kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako