• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Morocco yakamata kikundi cha magaidi kinachohusiana na kundi la IS karibu mpaka wa Algeria

    (GMT+08:00) 2016-06-25 18:49:17

    Idara ya usalama ya Morocco imekamata kikundi cha magaidi chenye watu kumi kinachohusiana na kundi la IS karibu na mpaka wa Algeria.

    Wizara ya mambo ya ndani ya Morocco imetoa taarifa ikisema, watuhumiwa hao walikuwa wanachunguza jumba kubwa la maduka huko Oujda ili kufanya uporaji kwa ajili ya kufadhili shughuli za kigaidi nchini humo, vitendo ambavyo vinafuatana na ajenda ya kundi la IS.

    Taarifa pia inasema, uchunguzi umeonesha kuwa kikundi hicho ambacho kilikutana mara kadhaa kisirisiri huko Oujda, kilishambulia raia wa kawaida na kupora mali zao.

    Morocco inakabiliwa na tishio linaloongezeka kutoka kundi la IS. Mkurugenzi wa idara kuu ya uchunguzi wa kisheria ya Morocco Abdelhak El Khayam alisema nchi hiyo imekamata vikundi 29 vya magaidi vilivyopanga mashambulizi nchini humo ndani ya mwaka mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako