• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China Li Keqiang akutana na rais Vladimir Putin wa Russia

    (GMT+08:00) 2016-06-26 16:51:01

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana hapa Beijing amekutana na rais Vladimir Putin ambaye yuko ziarani nchini China.

    Bw. Li Keqiang amesifu uhusiano wa sasa kati ya China na Russia na maendeleo yaliyopatikana kwenye ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na kusema kuwa China inapenda kuendelea kuimarisha uaminifu wa kisiasa na upande wa Russia, kukuza ushirikiano halisi kwenye sekta mbalimbali, kuhimiza mawasiliano ya kiraia kati ya nchi hizo mbili na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya China na Russia.

    Kwa upande wake rais Putin amesema, uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya Russia na China ambao ni wa pande zote na wenye nguvu, umekua kwa kasi na una mustakbali mkubwa. Amesema, Russia inapenda kuimarisha ushirikiano wa China kwenye sekta mbalimbali, haswa katika ujenzi wa umoja wa kiuchumi wa Ulaya na Asia na ujenzi wa ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako