• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 16 wauawa katika shambulizi dhidi ya hoteli nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2016-06-26 17:48:31

    Watu zaidi ya 16 wameuawa akiwemo waziri wa mambo ya mazingira wa Somalia na wengine wengi wamejeruhiwa katika milipuko miwili ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari iliyotokea jana alasiri kwenye hoteli moja katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

    Ofisa wa polisi nchini Somalia Mohamed Nor aliyeshuhudia shambulizi hilo amesema, wengi wa waliouawa ni raia wa kawaida waliokuwa katika hoteli ya Nasa-Hablod wakati milipuko ilipotokea.

    Kundi la Al-Shabaab limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako