• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IOM yaongeza juhudi za kukabiliana na Malaria Bentiu, Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2016-06-26 18:01:26

    Shirika la uhamiaji duniani IOM linasema limeongeza raslimali ili kukabiliana na maambukizi ya maradhi ya Malaria kwenye kituo cha kulinda raia cha Bentiu nchini Sudan Kusini.

    IOM inasema kuongezeka kwa maambukizi ya maradhi hayo kunatokana na msimu wa mvua inayopelekea kuongezeka kwa mbu.

    Mratibu wa masuala ya dharura ya kiafya kwenye shirika hilo Andrew Mbala amsema kwamba katika wiki mbili za kwanza za mwezi huu idadi ya maambukizi ya malaria kwenye kituo hicho iliongezeka zaidi ya maradufu, huku asilimia 50% ya wagonjwa wote kwenye zahanati mbili wakiwa ni wa Malaria.

    Mbala amesema ili kupunguza msongamano kwenye zahanati IOM inapanga kujenga vituo vya muda ili kuwawezesha watu kupata huduma za matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako