• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamanda wa jeshi la Iraq atangaza kukomboa Fallujah kutoka kwa kundi la IS

    (GMT+08:00) 2016-06-26 18:09:44

    Kamanda wa operesheni za ukombozi wa Fallujah, Luteni Jenerali Abdul-Wahab al-Saadi ametangaza ukombozi kamili wa mji wa Fallujah kutoka kwa wapiganaji wa kundi la IS baada ya mapigano yaliyodumu kwa mwezi mmoja dhidi ya kundi hilo lenye msimamo mkali.

    Al-Saadi amesema, jeshi la Iraq liliingia katika sehemu ya Golan iliyoko kaskazini magharibi mwa Fallujah, ambayo ilikuwa eneo la mwisho lililokombolewa kutoka kwa wapiganaji wa IS mjini humo.

    Taarifa kutoka ofisi ya habari ya kituo cha uongozi wa operesheni za pamoja za Iraq imethibitisha habari hiyo na kusema kundi la wanamgambo liitwalo Hashd Shaabi linafanya msako dhidi ya wapiganaji wa IS waliosalia mjini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako