• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha anga kilichobebwa na roketi ya Changzheng No. 7 charudi ardhini kwa usalama

    (GMT+08:00) 2016-06-26 18:34:18

    Sehemu ya kurudi duniani ya chombo cha safari za anga kilichorushwa jana usiku kwa kutumia roketi ya Changzheng No. 7 imerudi ardhini kwa usalama leo alasiri kwenye eneo la jangwa la gobi, kusini magharibi mwa China.

    Sehemu hiyo ya kurudi duniani yenye uzito wa tani 2.6 iliyosanifiwa kufanya majaribio ya teknolojia za safari za anga, imesafiri kwa masaa 20 kwenye njia yake ya kuzunguka dunia.

    Ofisa wa miradi ya safari za anga za juu ya China amesema, kurudi salama kwa chombo hicho kumeweka msingi muhimu kwa kazi za kusanifu na kuendeleza teknolojia muhimu za vyombo vipya vya anga za juu vinavyobeba wanaanga, na pia kunamaanisha kuwa malengo yaliyowekwa ya urushaji wa kwanza wa roketi ya Changzheng No. 7 yote yamefikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako