• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iceland yafikia robo fainali EURO baada ya kuitinga England

    (GMT+08:00) 2016-06-28 09:14:58

    Iceland imeiadhibu England mabao 2-1 na hivyo kusonga mbele hadi robo fainali kwenye michuano ya EURO 2016.

    Mchezo huo ulichezewa katika uwanja wa Stade de Nice.

    Wyne Rooney ndiye alieanza kwa kufunga penalty dakika ya nne, lakini sekunde 34 tu baadaye Ragnar Sigurdsson akasawazisha na kufanya mambo kuwa 1-1.

    Kunako dakika ya 18 Kolbeinn Sigthorsson aliweka Iceland kifua mbele kwa bao la pili na hali ikasalia hivyo mpaka kipenga cha mwisho.

    Baada ya kipigo hicho maneja wa England Roy Hodgson amejiuzulu.

    Na kwingineko kwenye EURO Hispania wamekubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa Italia, magoli ambayo yalianza kufungwa dakika ya 33 na Giorgia Chiellin na Graziano Pelle dakika ya 90.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako