• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza kuunga mkono mafungamano ya jumuiya ya EAC

    (GMT+08:00) 2016-06-29 10:20:47

    China imesisitiza kuunga mkono mchakato wa mafungamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC kwenye mambo ya reli, ndege na viwanda. Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Yongqing amesema hayo huko Arusha wakati alipokutana na katibu mkuu wa Jumuiya ya EAC balozi Liberat Mfumukeko.

    Balozi Lu amesisitiza haja ya jumuiya ya EAC ya kufuatilia kusainiwa kwa makubalino ya ushirikiano kwenye sekta ya anga kati ya China na jumuiya ya EAC, na kusema China inapenda kuimarisha ushirikiano na jumuiya ya EAC, hasa kwenye ujenzi wa eneo la biashara huria, ambao utasaidia bidhaa za jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye soko la China, hasa mazao ya kilimo.

    Mabalozi hao wawili pia wamejadili maeneo mengine yenye uwezekano wa ushirikiano, na haja ya kuandaa mikutano ya uwekezaji nchini China inayoongozwa na baraza la biashara la jumuiya ya Afrika mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako