• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ureno yaishinda Poland kwa 5-3 katika EURO 2016

    (GMT+08:00) 2016-07-01 09:48:12

    Mechi ya kwanza ya robo fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya ilichezwa jana kati ya Poland na Ureno. Baada ya dakika 120 kwisha kwa kufungana goli moja kwa moja, pande mbili zilipigiana mikwaju ya penati na hatimaye Ureno ikaibuka washindi kwa ushindi wa penati 5 kwa 3. Kwa matokeo hayo Ureno imekuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza nusu fainali.

    Leo timu ya Wales inapambana na timu ya Ubelgiji, kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali ambao unatarajiwa kuwa mgumu, hasa ikingatiwa kuwa Wales wameshangaza wengi, na kuwa ni timu pekee kati ya timu tatu za Uingereza zilizoingia kwenye michezo hiyo na kufika hatua ya robo fainali. Ubelgiji ni moja ya timu inayopigiwa upatu kuwa bingwa wa mshinda haya kwa mwaka huu, kutokana na kuwa na kikosi chenye nguvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako