• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Malighafi mpya ya kutengeneza skrini nzuri zaidi zinazoweza kupinda

    (GMT+08:00) 2016-07-01 13:54:10

    Skrini zinazoweza kupinda zimeanza kutumiwa katika baadhi ya vyombo vya elektroniki vikiwemo simu za mkononi. Lakini bado hazitumiwi kwa wingi kwa sababu sifa yake hairidhishi. Hivi karibuni watafiti wa Uingereza wametengeneza skrini nzuri zaidi kwa malighafi ya Graphene.

    Tofauti na skrini za zamani zilizotengenezwa kwa vioo, skrini hizi zinazotengenezwa kwa plastiki nyepesi zinaweza kupinda, lakini tatizo ni kwamba skrini hizi zikiwa kubwa, haziwezi kutoa mwangaza sawasawa katika sehemu zote.

    Ili kutatua tatizo hili, mwaka 2012 kikundi cha utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Exeter cha Uingereza kilitengeneza malighafi mpya iitwayo GraphExeter kwa kuweka tabaka la Ferric Chloride kati ya matabaka mawili ya Graphene. Malighafi hiyo ni angavu, nyepesi na inaweza kupinda kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko malighafi za zamani.

    Hivi karibuni kikundi hiki kimethibitisha sifa ya malighafi hii, na kutengeneza kwa mara ya kwanza skrini inayoweza kupinda kwa malighafi hiyo. Si kama tu skrini ya aina mpya inatoa mwangaza sawasawa katika sehemu zote, bali pia inatumia nishati chache.

    Dr. Saverio Russo wa kikundi hiki alisema utafiti wao umethibitisha kuwa malighafi hii inafaa kutengeneza skrini kubwa zaidi zinazoweza kupinda, huenda ikahimiza mabadiliko ya vyombo vya elektroniki, na kutumiwa kwa wingi katika mambo ya matibabu katika siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako