• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serengeti Boys yaiadhibu Shelisheli 6-0

    (GMT+08:00) 2016-07-04 09:10:02

    Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeshinda mabao 6-0 dhidi ya Shelisheli katika mchezo wa marudiano wa raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za vijana U17 Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Madagascar.

    Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inasonga mbele na kwenda raundi ya Pili na hatua ya mwisho ya mchujo kwa ushindi wa jumla wa mabao 9-0 baada ya wiki iliyopita kushinda 3-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.

    Serengeti Boys sasa itamenyana na Afrika Kusini, ikumbukwe hiyo ni kama marudio ya mchezo wa mwaka jana katika hatua hiyo hiyo, ambayo vijana wa Tanzania walitolewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako