• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cristiano Ronaldo aipaisha Ureno kwenye fainali za mataifa ya Ulaya 2016

    (GMT+08:00) 2016-07-07 08:12:39

    Jana usiku michuano ya mataifa ya Ulaya 2016 maarufu kama Kombe la Euro, iliendelea tena baada ya kusimama kwa mapumziko ya siku mbili, usiku huo ulishuhudiwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Euro 2016 kwa kuzikutanisha timu za taifa za Ureno dhidi ya Wales.

    Ureno ambayo mara ya mwisho kufungwa na Wales ilikuwa May 12 1951 katika mchezo wa kirafiki, ilifanikiwa kuitoa Wales kwa kuifunga jumla ya magoli 2-0, magoli ya Ureno yalifungwa kuanzia dakika ya 50 na Cristiano Ronaldo kwa kichwa, kabla ya dakika 3 baadae Luis Nani kupachika goli la pili kwa kutumia vyema uasaidizi wa Ronaldo.

    Kwa ushindi huo Cristiano Ronaldo ambaye ndio mchezaji bora wa mechi hiyo, anakuwa amefikia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote iliyokuwa inashikiliwa na Michael Platini ya kufunga jumla ya magoli 9, Ronaldo ana nafasi ya kuvunja rekodi hiyo endapo katika mchezo wa fainali atakaocheza na mshindi kati ya Ufaransa na Ujerumani kufunga goli moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako