• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha uchunguzi kiitwacho Juno kitachunguza nini katika sayari ya Jupiter? Unajua hadithi kuhusu sayari hiyo?

    (GMT+08:00) 2016-07-11 15:28:07

    Chombo cha uchunguzi kiitwacho Juno kilichorushwa na NASA kimeingia kwenye mzingo wa sayari ya Jupiter. Mkuu wa NASA Bw. Charles Bolden amefahamisha kuwa kupitia chombo hiki wanaweza kuchunguza ukanda mkubwa wenye mionzi kando ya Jupiter, kutafiti sehemu ya ndani ya sayari hii, kufahamu jinsi sayari hiyo ilivyopatikana na mabadiliko ya mfumo wa jua.

    Jupiter ni sayari maalum katika mfumo wa jua, kwani ni kubwa zaidi kuliko sayari nyingine, na uzito wake ni mara 2.5 ya uzito wa sayari nyingine zote. Aidha, ina satilaiti zaidi ya 60. Mfumo wake unafanana na mfumo mdogo wa jua.

    Hii ni sayari inayoundwa na hewa, hivyo baadhi ya hewa zilizokuwepo wakati mfumo wa jua ulipoundwa bado ziko juu yake, lakini hazikuwepo katika dunia yetu. Kutafiti hewa hizi kunasaidia kufahamu chanzo cha mfumo wa jua.

    Kama hupendi sana kusikiliza mambo ya kisayansi, basi pengine utapenda kusikia hadithi za kale kuhusu sayari hiyo. Jupiter ni jina la mungu wa kirumi, na katika hadithi za kigiriki pia anaitwa Zeus. Juno ndiye mke wake. Jupiter anajificha mawinguni, na ni mke wake tu anayeweza kuona sura yake halisi. Hii huenda ndio sababu ya chombo cha utafiti kupewa jina la Juno. Lakini tuangalie baadhi ya majina ya satilaiti za Jupiter, kwa mfano, majina ya wasichana Io, Europa, Callisto, Leda, Metis, n.k. Kwa mujibu wa hadithi za kale, makumi ya wasichana hao ni wapenzi wa Jupiter. Hivyo mke wake Juno akifika, jambo gani litatokea?

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako