• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwa nini wakati ukiwa na shughuli nyingi zaidi unapata uzito haraka zaidi?

    (GMT+08:00) 2016-07-08 07:25:08

    Kutokana na kuwa na kazi nyingi kunatufanya tule chakula kingi zaidi katika kila mlo, tukae mbele ya komputa kwa muda mrefu, na tunywe pombe nyingi.

    Utafiti mmoja umeonyesha kuwa watu huongeza uzito zaidi baada ya kufanya kazi miaka 3 tangu wahitimu na waandishi wa habari, wafanyakazi wa fani ya IT, madaktari na wanasheria huweza kupata uzito rahisi zaidi.

    Kama ukikaa siku zote au huwezi kulala kwa masaa ya kutosha utanenepa kirahisi zaidi, uchunguzi mmoja umeonyesha kwamba hatari ya kunenepa kwa watu ambao hawawezi kulala vizuri na kulala kwa saa za tosha ni asilimia 50 zaidi kuliko wanaoweza kulala kwa saa za kutosha.

    Na pia kula kidogo katika mlo wa asubuhi na kula vyakula vya kutengeza mwenyewe haraka kwa chakula cha mchana na kula kingi zaidi baada ya kufanya kazi usiku, kula kwa namna hiyo, bila shaka kunanenepesha.

    Madaktari wanatoa ushauri ufuatao

    Kwanza ni kulala mapema na kuamka mapema ili uwe na wakati wa kutosha wa kula chakula cha asubuhi na unaweza kula mayai, nyama ya ng'ombe, ndizi na kunywa maziwa kidogo ambavyo ni vyakula vinavyoweza kupunguza shinikizo lako.

    Pili ni kufanya mazoezi kidogo hata kama uko ofisini, unaweza kutembea kidogo kila baada ya dakika arobaini au hamsini na kunyoosha mwili wako kidogo.

    Tatu ni kujifurahisha mwenyewe, kwani unahitaji kujua kwamba lazima uwe na furaha ambayo itasaidia kupunguza uzito wako, kusoma vichekesho kidogo pia kutasaidia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako