• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujerumani yalimezea mate kombe la la Euro 2016  baada yakuchapwa 2-0 na Ufaransa

    (GMT+08:00) 2016-07-08 08:55:52

    Ujerumani jana usiku ilishuhudiwa ikibaki kulimezea mate kombe la Euro 2016 kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili walipocheza na timu mwenyeji Ufaransa katika uwanja wa Stade Velodrome baada ya kurambishwa nyasi na kukubali kichapo cha magoli 2-0. Huu ni mchezo ambao timu zote mbili zilikuwa zinapewa nafasi ya kushinda, ila Ufaransa walikuwa wana rekodi ya kuifunga Ujerumani mara 13, kupoteza mara 10 na sare mara 5, hiyo ni takwimu kwa mujibu wa mechi zao 28 walizowahi kucheza toka March 5 1931. Rekodi hiyo pamoja na uenyeji ukafanikisha kuisaidia Ufaransa kuibuka na ushindi huo, ambao uliisaidia timu hiyo kutinga katika hatua ya fainali katika ardhi ya kwao, magoli yote yaUfaransa yalifungwa na Antoine Griezmann dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 72, Ufaransa sasa watacheza na Ureno katika mchezo wa fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako