• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Daraja la kuning'inia lililojengwa na kampuni ya China lazinduliwa Morocco

    (GMT+08:00) 2016-07-08 19:34:02

    Mfalme Mohammed VI wa Morocco amezindua daraja lililojengwa na kampuni ya China ambalo ni kubwa zaidi la kuning'inia barani Afrika.

    Mfalme huyo amewashukuru wafanyakazi wa China na kusema ujenzi huo umetimiza ndoto ya watu wa Morocco ya miaka 30 iliyopita.

    Daraja hilo lenye urefu wa mita 952 na upana wa mita 30.4 linaunganisha mji mkuu wa Morocco Rabat na mji wa kaskazini magharibi Sale, na ni daraja la kwanza la kisasa la aina hiyo barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako