• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ureno ndio mabingwa wa Euro 2016

    (GMT+08:00) 2016-07-11 09:19:58

    Ureno ndio mabingwa wa michuano ya kandanda ya Ulaya, Euro 2016, baada ya kuwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika dakika za ziada kwenye mchezo wa fainali uliochezewa mjini Paris.

    Goli la ushindi hilo lilitiwa kimyani na Éderzito António Macedo Lope maarufu kama Eder katika dakika ya 110, mbele ya umati mkubwa wa mashabiki waliofurika kujionea fainali hiyo kwenye uwanja wa Stade de France.

    Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano bila ya mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo aliyetoka kutokana na kupata jeraha la goti katika kipindi cha kwanza.

    Ufaransa ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini hawakuweza kuzitumia vyema nafasi walizopata na hivyo kuwawezesha Ureno kuandikisha historia hili likiwa ndilo kombe lao kubwa zaidi la kimataifa kuwahi kushinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako