• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watafiti wagundua kuwa kimondo kiligonga dunia na kusababisha kutoweka kwa viumbe vya baharini

    (GMT+08:00) 2016-07-11 15:28:58

    Watafiti wa Japan wametoa ripoti kwenye gazeti la Ripoti za Sayansi la Uingereza wakisema wamegundua ushahidi kwamba katika miaka milioni 215 iliyopita kimondo kiligonga dunia na kusababisha kutoweka kwa viumbe vya baharini.

    Watafiti wa Chuo Kikuu cha Kumamoto cha Japan na idara ya utafiti na uendelezaji wa bahari ya Japan waligundua ushahidi wa kimondo kugonga dunia katika miaka milioni 237 hadi 200 iliyopita huko kaunti ya Gifu, na wamekadiria kuwa kipenyo cha kimondo hiki ni mita 2.2 hadi 7.8.

    Watafiti pia wamekusanya mabaki ya wadudu wadogowadogo baharini katika zama za kale wenye ukubwa usiozidi milimita 1. Baada ya kutafiti mabaki hayo, watafiti wamegundua kuwa baada ya kimondo kugonga dunia, mimea midogomidogo ya baharini ambayo ni chakula cha wadudu ilipungua kwa kiasi kikubwa, na kusababisha wadudu kutoweka kwa wingi katika miaka milioni 215 iliyopita.

    Kabla ya hapo, watafiti waliwahi kutafiti tu tukio la kutoweka kwa dinosaur katika miaka milioni 66 kutokana na vimondo kugonda dunia. Tukio hili la kutoweka kwa viumbe vya baharini lilitokea zamani zaidi. Watafiti wataendelea kutafiti athari ya tukio hili kwa viumbe vinavyoishi katika nchi kavu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako