• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Roboti ya kumwua mtu" ya Marekani yasababisha wasiwasi

    (GMT+08:00) 2016-07-13 10:30:29

    Baada ya tukio la kuwashambulia polisi kutokea huko Dallas, Marekani, idara ya polisi imethibitisha kuwa mshambuliaji Micah Johnson aliuawa na roboti ya bomu. Hii ni mara ya kwanza kwa polisi wa Marekani kumwua mhalifu kwa roboti. Ingawa si nadra kwa polisi wa Marekani kutumia roboti katika kazi zao, lakini "roboti hii ya kumwua mtu" imesababisha wasiwasi kwa watu kuhusu sheria na maadili, hata wasiwasi kuhusu roboti.

    Ukweli ni kwamba roboti za mabomu zimetumiwa na polisi wa Marekani katika miaka mingi iliyopita. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwaka jana na Chuo cha Bard cha Marekani, idara 200 hivi za utekelezaji wa sheria zina roboti hizi. Roboti inayotumiwa na polisi wa Dallas ni aina ya MARCbot-IVs ambayo ilitengenezwa na kampuni ya Exponent.

    Kuhusu roboti zinazotumiwa na jeshi, watu wana wasiwasi kama zitaongeza hatari ya kutokea kwa vita. Na kuhusu roboti zinazotumiwa na polisi, watu wanafikiri huenda zitawasababisha polisi kuchukua hatua kali kupita kiasi.

    Bw. William Cohen ambaye aliwahi kushiriki kwenye usanifu wa roboti hii anaona kuwa uamuzi wa polisi wa Dallas umezua masuali mbalimbali yakiwemo katika hali gani polisi wanaweza kuacha mazungumzo na kuwaua wahalifu kwa roboti hii.

    Roboti iliyotumiwa na polisi wa Dallas haiwezi kuua watu yenyewe, bali ilidhibitiwa na polisi, hivyo kauli kuhusu tishio la roboti kwa maisha ya binadamu ni uwongo. Prof. Ryan Calo wa Chuo Kikuu cha Washington amesisitiza kuwa "roboti ya kumwua mtu" na "kumwua mtu kwa roboti" ni mambo mawili tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako