• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Standard ya Afrika Kusini kubadilisha sarafu ya China nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2016-07-14 10:33:00

    Benki ya Standard ya Afrika Kusini ambayo ni benki kubwa zaidi barani Afrika imezindua huduma ya kubadilisha sarafu ya China RMB huko Nairobi Kenya, na kuwa benki ya kwanza nchini Kenya kutoa huduma hiyo.

    Baada ya kubadilisha RMB 1,000 kuwa shilingi za Kenya, balozi wa China nchini Kenya Bw. Liu Xianfa amesema kuzinduliwa kwa huduma kumewezesha ubadilishanaji huru wa sarafu ya China nchini kenya, na hatua hiyo ina maana kubwa katika kukuza kwa kina zaidi ushirikiano kati ya China na Kenya katika nyanja mbalimbali.

    China imekuwa mwenzi wa kwanza wa biashara wa Kenya na bara zima la Afrika. Balozi Liu amesema kuongezeka kwa biashara na uwekezaji wa China nchini Kenya kumeweka msingi imara kwa huduma hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako