• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SIMBA XV ya Kenya yajinoa kisawasawa kukabiliana na mabingwa watetezi Namibia

    (GMT+08:00) 2016-07-15 10:07:34

    Timu ya raga ya Kenya ya wachezaji 15 kila upande SIMBA XV, iko tayari kukabiliana na mabingwa watetezi Namibia katika mechi yao ya pili ya Kombe la Afrika uwanjani Hage Geingob jijini Windhoek hapo kesho Julai 16. Mabingwa hawa wa Afrika mwaka 2011 na 2013 walikamilisha maandalizi yao Alhamisi na kocha Jerome Paarwater leo amepanga kutaja kikosi kitakachoanza mechi ya Namibia. Kenya inaongoza mashindano haya kwa ubora wa magoli baada ya kuwapepeta mabingwa wa 2010 na 2012 Zimbabwe 61-15 mnamo Julai 9 jijini Harare katika mechi yao ya ufunguzi.

    Namibia pia ilianza kampeni yake kwa ushindi wa 40-31 dhidi ya Uganda mnamo Julai 2 jijini Kampala. Mshindi kati ya Kenya na Namibia atakuwa na nafasi kubwa ya kuibuka bingwa wa Afrika mwaka 2016. Wenyeji Namibia na wageni wao Kenya wanatarajiwa kutangaza vikosi vyao leo hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako