• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sayari kibete Pluto yapata "mwenzi mpya"

    (GMT+08:00) 2016-07-15 10:22:48

    Sayari kibete Pluto ambayo iliwahi kuchukuliwa kama sayari imepata "mwenzi mpya". Kikundi cha wanajimu cha kimataifa hivi karibuni kimetangaza kuwa kimegundua sayari kibete mpya inayosafiri kwa mzingo mrefu zaidi katika ukanda wa Kuiper ulioko nje ya mzingo wa sayari ya Neptune.

    Wanajimu walipotekeleza mradi wa uchunguzi wa chanzo cha mfumo wa nje wa jua kupitia darubini ya uchunguzi wa anga ya juu ya Canada-Ufaransa-Hawaii iliyoko huko Hawaii Marekani, waligundua sayari kibete mpya. Sayari kibete hii imepewa jina la "2015 RR245" na Shirika la Unajimu la Kimataifa.

    RR245 ina kipenyo cha kilomita 700, inahitaji miaka 700 kuzunguka jua kwa mzingo mmoja, muda huo ni mrefu zaidi kuliko sayari kibete nyingine. Kwa mfano, Pluto inahitaji miaka 248 kuzunguka jua kwa mzingo mmoja.

    Sasa RR245 inaelekea sehemu iliyoko karibu kabisa na jua kwenye mzingo wake, ambayo iko umbali wa kilomita bilioni 5 kutoka jua, na inakadiriwa kufika huko mwaka 2096. Watafiti wamesema ugunduzi wa sayari kibete hii utawasaidia binadamu kutafiti chanzo cha mfumo wa jua.

    Kabla ya hapo, Shirka la Unajimu la Kimtaifa limeidhinisha sayari kibete tano, zikiwemo Ceres, Pluto, Haumea, Makemake na Eris.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako