• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sayari inayozunguka "majua" matatu yagunduliwa

    (GMT+08:00) 2016-07-15 10:23:14

    Wanajimu wamegundua sayari inayozunguka nyota tatu kupitia darubini ya VLT iliyoko katika kituo cha uchunguzi wa anga ya juu cha kusini cha Ulaya. Zamani wanajimu walifikiri njia ya kuzunguka nyota tatu haiwezi kudumu, na sayari huenda ikaondoka haraka. Lakini sayari hii inaendelea kufuata njia hii. Ugunduzi huu unaonesha kuwa sayari zinazozunguka nyota tatu pengine sio nadra sana.

    Sayari hii iitwayo HD 131399Ab iko umbali wa miaka 320 ya kusafiri kwa mwanga kutoka duniani, na iko katika kundi la nyota la Centaurus. Sayari hiyo yenye umri wa miaka milioni 16 ni moja kati ya sayari zenye umri mdogo zaidi nje ya mfumo wa jua, na pia ni moja kati ya sayari zilizopigwa picha na binadamu. Joto kwenye sayari hiyo ni nyuzi 580 sentigredi, na uzito wake ni mara 4 ya sayari ya jupiter, hivyo hii pia ni sayari yenye baridi na nyepesi zaidi nje ya mfumo wa jua iliyopigwa picha na binadamu.

    Mgunduzi wa sayari hiyo Kevin Wagner kutoka Chuo Kikuu cha Arizona amesema muda wa mzunguko mmoja wa sayari hii ni miaka 550. Katika nusu ya muda huo "majua" matatu yanaonekana angani kwenye sayari hiyo, na kuna mchana na usiku; na wakati sayari hii inaposafiri katikati ya sayari hizi, "jua" kubwa linapochomoza, "majua" mengine mawili madogo yanatua, na siku nzima inakuwa mchana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako