• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rasilimali mpya inatazamiwa kufanya kila kitu kiwe skrini

    (GMT+08:00) 2016-07-18 15:22:15

    Kikundi cha utafiti cha Japan kimevumbua rasilimali mpya ambayo inaweza kukatwa kwenye maumbo mbalimbali, na kubandika juu ya miavuli, magari, majengo n.k., na kuvifanya vitu vyote kuwa skrini.

    Skrini za kawaida zimetumiwa kwa wingi katika bidhaa za elektroniki zikiwemo simu za mkononi. Katika miaka ya hivi karibuni, watu wanatengeneza skrini nyingi zaidi zinazoonesha matangazo na bidhaa za elektroniki zinazovaliwa mikononi, mahitaji kuhusu rasilimali mpya ya kutengeneza skrini yameongezeka. Lakini skrini za jadi haziwezi kukatwa baada ya kumaliza kutengenezwa, na zinahitaji kuunganishwa na umeme wakati wote zinapofanya kazi, hivyo hazifai kutumiwa katika mazingira mbalimbali.

    Rasilimali mpya iliyovumbuliwa na watafiti wa Japan ni mchanganyiko wa kemikali za kaboni na metali. Inaweza kukatwa kama unavyopenda kwa mikasi, na ikiunganishwa na umeme kwa sekunde chache tu, rangi yake inabadilika, tena rangi hii itadumu baada ya kutolewa kwenye umeme.

    Kikundi hiki kinasema katika siku zijazo kitajaribu kuvumbua rasilimali inayoweza kutengeneza skrini kubwa zaidi na kuonesha rangi nyingi zaidi, na kutarajia kuwa maandishi na picha zitaweza kuoneshwa kwenye mahali na vitu mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako