• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika asema China ni mwenzi muhimu wa kimkakati wa Afrika

    (GMT+08:00) 2016-07-16 18:10:36

    Naibu mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Erastus Mwencha amesema, China ni mwenzi muhimu wa kimkakati wa Afrika na kwamba bara hilo linanufaika katika ushirikiano kati yao wa biashara, afya na usalama.

    Bw. Mwencha amesema, biashara kati ya China na Afrika imeongezeka kwa kasi na thamani yake imefikia zaidi ya dola za Marekani bilioni 200. Amesema China imesaidia nchi za Afrika kushinda vita dhidi ya Ebola na kupanga kujenga kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika na pia kushiriki kwenye operesheni ya kulinda amani na kufanya ushirikiano kwenye sekta ya usalama barani humo..

    Naye kamishina wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya miundombinu na nishati Bibi Elham Mahmood Ibrahim amesema, China imefanya kazi muhimu katika kuwezesha Afrika kutumia ipasavyo nguzu zake katika sekta za nishati na miundombinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako