• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba na Yanga kukutana Oktoba Mosi mwaka huu

    (GMT+08:00) 2016-07-20 08:54:41
    Watani wa jadi Simba na Yanga watakutana Oktoba 1 mwaka huu katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Kwa mujibu wa Ratiba ya Ligi Kuu iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) michuano hiyo itaanza Agosti 20 kwa mechi saba kuchezwa kwenye viwanja tofauti, ikitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Mechi za ufunguzi za Ligi Kuu Agosti 20, Simba SC watacheza na Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Azam wakiikaribisha African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako