• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha Stars dhidi ya Nigeria kutajwa kesho

    (GMT+08:00) 2016-07-25 09:14:24

    Kocha MkuuTaifa Stars Charles Mkwasa wiki ijayo anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

    Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, kambi hiyo itaingia kambini Agosti 01 na Mkwasa amelenga kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji katika kambi hiyo ambayo itakuwa ya awali.

    Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako