• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Facebook yafanikiwa kufanya majaribio ya ndege isiyo na rubani inayotumia nishati ya jua

    (GMT+08:00) 2016-07-26 07:37:59

    Kampuni ya Facebook hivi karibuni imetangaza kuwa imefanikiwa kufanya majaribio ya kwanza ya ndege isiyo na rubani iitwayo Aquila inayotumia nishati ya jua.

    Hivi sasa watu bilioni 4 hivi duniani bado hawajaunganishwa na mtandao wa Internet. Mwaka 2014, kampuni hiyo ilianzisha maabara ya uunganishaji, ambayo inalenga kutoa huduma ya mtandao wa Internet kupitia ndege zisizo na rubani, satilaiti na mifumo ya mawasiliano ya simu

    Tarehe 28 maabara hiyo ilifanya majaribio ya kwanza ya ndege ya Aquila huko Arizona, Marekani. Kiunzi cha ndege hii kilitengenezwa kwa nyuzi za kaboni, upana wa mabawa yake ni mkubwa kuliko ndege ya abiria ya Boeing 737, lakini uzito wake ni theluthi moja ya gari la nishati ya umeme. Ndege hiyo inaweza kuruka angani kwa miezi mitatu mfululizo, lakini inatumia nishati chache tu ambayo ni sawa na nishati inayotumiwa na vyombo vitatu vya kukausha nywele au maikrowevu moja.

    Kwa mujibu wa mpango, ndege hiyo inaweza kuzunguka eneo lenye kipenyo cha kilomita 97, na kutoa ishara ya mtandao wa Internet kutoka anga yenye urefu wa kilomita 18 kwa mifumo ya mwangaza leza na mawimbi ya masafa ya milimita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako